
[2.61] Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumiliachakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wakoMlezi atutolee vile vinavyo mea katika ardhi, kamamboga zake, na matango yake, na thom zake, na adesizake, na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili kilichoduni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko mtapatamlivyo viomba. Na wakapigwa na unyonge,na umasikini,na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya nikwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasipo haki. Hayo ni kwawalivyo asi na wakapindukia mipaka.
[2.177] Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wamashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muaminiMwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaana mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, nakatika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; haondio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.
|